• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 07, 2019

  SAMATTA ASHINDA TUZO YA 'KIATU CHA EBONY’ LIGI YA UBELGIJI, KOCHA BORA PIA GENK

  Na Mwandishi Wetu, BRUSSELS 
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta 'Samagoal' anayechezea KRC Genk ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Mwafrika katika Ligi ya Ubelgiji, ijulikanayo kama Jupiler Pro League. 
  Samatta ameshinda tuzo hiyo iitwayo 'Kiatu cha Ebony katika sherehe za tuzo za Jupiler Pro League usiku wa Jumatatu mjini ukumbi wa Birmingham Palace mjini Brussels.
  Samatta anakuwa mchezaji wa tatu tu wa Genk kushinda tuzo hiyo baadfa ya Oulare mwaka 1999 na Dagano mwaka 2002.
  Mbwana Samatta wa KRC Genk ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Mwafrika katika Jupiler Pro League 

  Pamoja na Samatta, Genk pia imetoa kocha Bora wa Msimu wa Jupiler Pro League, ambaye ni Kocha wake Mkuu, Mbelgiji Philippe Clement. 
  Nyota wengine wa KRC Genk walioingia kwenye kinyanganyiro lakini wakatoka kapa ni Malinovskyi na Pozuelo (Mchezaji Bora) na Promise (Sander Berge).
  Ikumbukwe Samatta ameshinda tuzo hiyo baada ya kazi nzuri msimu huu, akiisaidia Genk kukaribia kutwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
  Hadi sasa, Samatta tayari amefunga mabao 23 msimu huu na matatu katika Championship Round akiwa anaendelea kuongoza kwenye mbio za ufungaji bora. 
  Kwa ujumla, Samatta mwenye umri wa miaka 26, ameifungia Genk mabao 62 katika mechi 153 za mashindano yote tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amefunga mabao 47 katika mechi 120, kwenye Kombe la Ubelgiji amefunga mabao mawili katika mechi tisa na Europa League amefunga mabao 14 katika mechi 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ASHINDA TUZO YA 'KIATU CHA EBONY’ LIGI YA UBELGIJI, KOCHA BORA PIA GENK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top