• HABARI MPYA

  Wednesday, May 29, 2019

  JOSHUA AFANYA MAZOEZI YA WAZI NEW YORK KABLA YA KUMVAA RUIZ

  BINGWA wa ngumi uzito wa juu duniani, Anthony Joshua (kulia) amefanya mazoezi ya wazi leo mjini New York kuelekea pambano lake na Andy Ruiz Juni 1 mjini humo siku ambayo pia mabondia wa kike Delfine Persoon na Katie Taylor watapigana.
  Joshua mwenye urefu wa futi sita kwa sasa anashikilia mataji matatu kati ya manne; IBF, WBA na WBO akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake yote 22, kati ya 21 kwa knockout.
  Ruiz mwenye urefu wa futi nne amepoteza pambano
  moja na kushinda 32, huku 21 akishinda kwa knockout pia.
  Delfine Persoon wa Ubelgiji ndiye bingwa wa taji la WBC uzito wa Light na Katie Taylor wa Ireland anashikilia mataji ya WBA, IBF na WBO uzito huo wa Light PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA AFANYA MAZOEZI YA WAZI NEW YORK KABLA YA KUMVAA RUIZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top