• HABARI MPYA

  Thursday, May 16, 2019

  SIMBA SC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIA MTIBWA SUGAR 3-1 LEO DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 85 baada ya kucheza mechi 34 na kurudi juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiwazidi kwa pointi mbili mahasimu wao, Yanga SC.
  Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 49 baada ya kucheza mechi 36, ikibaki nafasi ya tano nyuma ya tano, nyuma ya KMC yenye pointi 49 pia za mechi 36.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Simba SC yamefunga na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya 33, kiungo Mzambia Clatous Chama dakika ya 48 na mshambuliaji Mganda Mganda Emmanuel Okwi.

  Simba SC ingeweza kuvuna ushindi mtamu zaidi leo kama si wachezaji wake, Adam Salmba kukosa bao la wazio kipindi cha pili.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Stand United imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
  Mabao ya Stand United yamefungwa na Charles Chinonso dakika ya tatu, Jackob Massawe dakika ya 48 na Datius Peter dakika ya 90 na ushei, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Khamis Khamis dakika ya 45.
  Mabao ya Stars United yamefungwa na Charles Chinonso dakika ya tatu, Jackob Massawe dakika ya 48 na Datius Peter dakika ya 90 na ushei, wakati la Kagera Sigar limefungwa na Khamis Khamis dakika ya 45. 
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalal’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni Jonas Mkude, Clatous Chama, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk81, John Bocco/Muzamil Yassin dk60, Meddie Kagere/Adam Salamba dk73 na Emmanuel Okwi.
  Mtibwa Sugar; Shaaban Kado, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Shabaan Nditi, Salum Kihimbwa/Salum Kihimbwa dk83, Ally Makarani, Jaffar Kibaya/Saleh Khamis dk70, Riphat Msuya na Haroun Chanogo/Ismail Aidan dk62.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIA MTIBWA SUGAR 3-1 LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top