• HABARI MPYA

    Monday, November 05, 2018

    THOMAS ULIMWENGU AVUNJA MKATABA NA EL HILAL YA SUDAN MIEZI MITANO TU TANGU ASAJILIWE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amevunja mkataba na klabu ya El Hilal ya Sudan, miezi mitano tu tangu ajiunge nayo akitokea AFC Eskilstuna ya Sweden.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online kwa simu, Ulimwengu amesema kwamba ameamua kuachana na El Hilal baada ya mambo kwenda tofauti alivyotarajia.
    “Kweli kaka, ninaondoka, mambo hayajakwenda kama nilivyotarajia, muda si mrefu nitakuambia ninakwenda wapi,”amesema Ulimwengu aliyejiunga na Hilal baada ya kuwa nje kwa muda mrefu sababu ya maumivu ya goti.



    Thomas Ulimwengu amevunja mkataba na El Hilal ya Sudan miezi mitano tu tangu ajiunge nayo

    Alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Taasisi ya Sayansi ya Michezo mjini Cape Town, Afrika Kusini mwaka jana na kupitia kipindi kirefu cha mazoezi ya kujiweka fiti.
    Ulimwengu alikwenda kwa watalaamu nchini Italia kufanyishwa mazoezi maalum ya kumuweka fiti haraka arejee uwanjani, ambayo hakika yamemsaidia na hadi kurudi uwanjani.
    Maumivu ya goti yamekuwa yakimsakama Ulimwengu tangu alipojiunga na Eskilstuna Januari mwaka jana akitokea Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kiasi cha kushindwa kucheza. 
    Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya AFC Eskilstuna ya Sweden, alikocheza hadi mwaka 2011  alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
    Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.
    Ulimwengu alihamia Ulaya baada ya kushinda mataji makubwa akiwa na  Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: THOMAS ULIMWENGU AVUNJA MKATABA NA EL HILAL YA SUDAN MIEZI MITANO TU TANGU ASAJILIWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top