• HABARI MPYA

    Tuesday, November 06, 2018

    BAKHRESA ATOA NDEGE YAKE BINAFSI KWA MARA YA KWANZA IWABEBE WACHEZAJI WA AZAM FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MFANYABIASHARA Bilionea, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa kwa mara ya kwanza jana alitoa ndege yake binafsi na familia yake iwabebe wachezaji klabu yake, Azam FC mjini Bukoba.
    Walikuwa ni wachezaji wake walioitwa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili wawahi kurejea Dar es Salaam kujiunga na wenzao kwa safari ya Afrika Kusini kambini.
    Hiyo ilikuwa mapema jana, yaani baada tu ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar walioshinda 1-0, bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma.
    Ndege ya Bilionea, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa ikiwa Uwanja wa Ndege wa Bukoba jana na wachezaji wa Azam FC

    Wachezaji hao ni mabeki Aggrey Morris, Abdallah Kheri, viungo Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji Yahya Zayed.
    Lakini pia katika ndege hiyo walikuwepo wachezaji wengine wa timu za taifa za nje, beki wa Uganda Nico Wadada na kiungo wa Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu waliokuja kuunganisha ndege Dar es Salaam kwenda kujiunga na timu zao.
    Walikuwepo pia kocha Hans van der Pluijm, Daktari Mwanandi Mwankemwa, wakati wachezaji wengine wote wamerejea kwa basi.
    Ni ndege ndogo inayoweza kubeba watu 13 ambayo kwa kawaida ni maalum ya mmiliki wa klabu, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake na kwa mara ya kwanza jana imetolewa kwa matumizi ya timu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAKHRESA ATOA NDEGE YAKE BINAFSI KWA MARA YA KWANZA IWABEBE WACHEZAJI WA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top