• HABARI MPYA

    Friday, October 02, 2015

    NDANDA KOSOVO TAABANI KITANDANI, ANATAPIKA DAMU NA...

    Pichani Ndanda akiwa amelazwa hospitali na picha ndogo ni matapishi ya damu
    MWIMBAJI na rapa maarufu hapa nchini, Ndanda Kosovo hali yake si shwari na amelazwa hospitali kwa maumivu ya tumbo yanayomsababishia kutapika damu. 
    Kwa mujibu wa Saluti5.com Ndanda aliyetesa na bendi ya FM Academia na Stono Musica, amelazwa katika hospitali ya PKA iliyoko Tegeta jijini Dar es Salaam. 
    Msanii huyo mcheshi ameimbia Saluti5 kwa njia ya simu kuwa amelazwa hapo tangu jana (Jumatano) ambapo tatizo kubwa ni kupasuka kwa mmoja ya mishipa tumboni. Ndanda amesema amekuwa akitapika damu, lakini madaktari wanajitahidi kudhibiti tatizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDANDA KOSOVO TAABANI KITANDANI, ANATAPIKA DAMU NA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top