• HABARI MPYA

    Sunday, October 11, 2015

    'MASHUSHU' WA ALGERIA WAKICHUKUA 'DATA' ZA TAIFA STARS LEO MALAWI

    Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya soka ya Algeria, Nabil Neghiz (kulia) akiwa na Meneja wa timu hiyo, Walid Sadi (kushoto) Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Malawi mchana wa leo kufuatilia mchezo wa marudiano hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi baina ya wenyeji na Tanzania waliofungwa 1-0. Hata hivyo, Taifa Stars imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya Jumatano kushinda 2-0 Dar es Salaam na sasa itamenyana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo Novemba.
    Nabil kulia akiandika mahitaji yake kwa ajili ya kupeleka ripoti nchini kwao, ili kuifanyia kazi kabla ya mchezo na Tanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'MASHUSHU' WA ALGERIA WAKICHUKUA 'DATA' ZA TAIFA STARS LEO MALAWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top