• HABARI MPYA

    Friday, April 17, 2015

    MAN UNITED KATIKA WAKATI MGUMU WAKIIVAA CHELSEA KESHO, NYOTA WANNE TEGEMEO NJE KWA MAJERUHI

    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney anaweza kuchezeshwa katika nafasi ya kiungo kesho Uwanja wa Stamford Bridge kutokana na Michael Carrick na Daley Blind kuwa miongoni mwa wachezaji wanne watakaosekana katika kikosi cha Manchester United kwenye ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea.
    Mabeki wa kati, Phil Jones na Marcos Rojo pia wataukosa mchezo huo dhidi ya vinara wa Ligi Kuu, na Jonny Evans atakuwa anakamilisha adhabu yake ya kufungiwa mechi sita, jambo ambalo limemfanya kocha Louis van Gaal, asema; 'Ni mtihani mgumu'.
    Jones na Blind, ambao waliumizwa na beki wa Manchester City, Vincent Kompany mwishoni mwa wiki, wote wana maumivu ya enka, wakati Carrick hakumaliza mchezo huo baada ya baada ya kuumia na Rojo baadaye akaripotiwa kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya tumbo.
    Phil Jones was replaced by Marcos Rojo last week and both are unavailable for Manchester United
    Phil Jones alimpisha Marcos Rojo wiki iliyopita na wote watakosekana kesho Manchester United
    Louis van Gaal puts his arm round Manchester United captain Wayne Rooney during training this week
    Louis van Gaal puts his arm round Manchester United captain Wayne Rooney during training this week

    Kocha Van Gaal amesema kwamba Rooney anaweza akacheza nafasi ya kiungo mkabaji dhidi ya Chelsea

    KIKOSI CHA MAN UNITED KESHO CHAWEZA KUWA...

    4-1-4-1: De Gea; Valencia, Smalling, Blackett, Shaw; Rooney; Mata, Herrera, Fellaini, Young na Falcao
    Tatizo la majeruhi United linamaanisha kwamba beki Luke Shaw na mshambuliaji Radamel Falcao wote wanweza kuanza kesho dhidi ya timu ya Jose Mourinho.
    "Tuna majeruhi wanne ambao walicheza mechi iliyopita, hivyo hiyo siyo nzuri kwetu,"amesema Van Gaal. "Tulikuwa tuna matumaini makubwa kwamba tunaweza kuwaponya wawili kati yao hao wanne, si hivyo. Carrick yuko nje na Rojo yuko nje, lakini pia Blind na Jones.
    "Hili ni pigo kubwa kwa sababu Rojo na Jones ni wazuri katika beki ya kati kushoto. Evans anatumikia adhabu, hivyo hatuna nafasi zaidi. Blind na Carrick wanaweza kucheza katika nafasi ya kiungo mkabaji, hivyo sina mchezaji mwingine, au Wayne Rooney anaweza kucheza katika nafasi hiyo,".
    Luke Shaw hasn't featured under Louis van Gaal recently but should return to play at left back
    Luke Shaw hajacheza chini ya Louis van Gaal, lakini anaweza kurejea katika beki ya kushoto

    Alipoulizwa kama Shaw anaweza kurejea kwa mara ya kwanza tangu atolewe katika mechi ya Kombe la FA wakifungwa na Arsenal mwezi uliopita baada ya kuumia, Van Gaal akajibu: "Labda utamuona kesho. Huwezi kujua. Luke yuko fiti kiasi cha kutosha nafikiri. Hajacheza kwa muda wa wiki kama wiki nne au tano, sipendi hali hiyo, lakini nafikiri yuko fiti kiasi cha kutosha,"amesema.
    Van Gaal pia amedokeza kwamba Robin van Persie anaweza kucheza kwa muda fulani, akisema: "Van Persie ni hadithi nyingine. Hii ni wiki ya kwanza amefanya mazoezi nasi, na kikosi cha kwanza, lakini labda tunaweza kumfikiria,".
    Chelsea ikiwa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi nane zaidi na mchezo mmoja mkononi, itawavaa United wanaoshika nafasi ya tatu kesho na Van Gaal anaamini kwamba Mourinho atafurahia hata sare.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED KATIKA WAKATI MGUMU WAKIIVAA CHELSEA KESHO, NYOTA WANNE TEGEMEO NJE KWA MAJERUHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top