• HABARI MPYA

  Thursday, December 18, 2014

  WATOZA USHURU KENYA WASAJILI WATANO, WAMTEMA MGANDA IVAN ANGUYO

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  KLABU ya ligi kuu ya taifa la Kenya, Ushuru FC imemtema aliyekuwa beki wa Gor Mahia na mganda Ivan Anguyo huku ikiwasajili wachezaji watano.
  Anguyo alijiunga na klabu hiyo inayofadhiliwa na Shirika la kutoza Ushuru nchini Kenya (K.R.A) msimu uliyopita kwa mwaka mmoja na sasa yupo huru kujiunga na klabu nyengine alivyothibitisha kocha mkuu Ken Kenyatta.
  “Anguyo yupo huru kuhamia klabu nyengine manake hatutampa mkataba mwingine baada ya wake wa mwaka mmoja kukamilika, Kenyatta aliliambia BIN ZUBEIRY.
  Samuel Odhiambo kulia ametua K.R.A.

  Kando na Anguyo, Ushuru pia wamemtupia virago mshambulizi na raia wa Nigeria Joseph Emeka ambaye amejiunga na klabu ya Shabana FC kwa mkataba wa miaka miwili.
  Hayo yakijiri, Ushuru imewasajili wachezaji watano. Hao ni Charles Okwemba kutoka AFC Leopards, mlindamlando Samuel ‘Abawa’ Odhiambo kutokea Tusker FC, Nelson Marasowe (Nairobi City Stars), Nelson Simwa (West Kenya Sugar) na Moses Arita Sengera ambaye hakukuwa na klabu baada ya kutemwa na Thika United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WATOZA USHURU KENYA WASAJILI WATANO, WAMTEMA MGANDA IVAN ANGUYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top