• HABARI MPYA

  Thursday, December 18, 2014

  POLISI YAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA, YATAKA MWILI UCHUNGUZWE KWANZA

  AISHA MADINDA SASA KUZIKWA KESHO …polisi wazuia mwili wake, kufanyiwa upasuaji mchana huu
  Mnenguaji Aisha Madinda aliyefariki jana asubuhi, atazikwa kesho mchana badala ya leo kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
  Mtoto wa kwanza marehemu, Feisal ameiambia Saluti5 kuwa polisi wamesema ni lazima mwili wa mama yake ufanyiwe upasuaji (postmortem) ili kujua chanzo cha kifo chake.
  Awali ndugu wa marehemu walisema hawahitaji Asha Madinda afanyiwe upasuaji, lakini baada ya polisi kutembelea eneo la tukio la kifo chake huko Mabibo, wamesema ni lazima upasuaji ufanyike.
  Feisal amesema upasuaji unatarajiwa kufanyika leo mchana hali inayowalazimisha kubadili ratiba ya mazishi.
  Aisha Madinda sasa atazikwa kesho mchana baada ya sala ya Ijumaa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI YAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA, YATAKA MWILI UCHUNGUZWE KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top