• HABARI MPYA

  Wednesday, December 17, 2014

  THIERRY HENRY APIGA BONGE LA BAO BAADA YA KUSTAAFU SOKA

  NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amekuwa mchambuzi wa soka anayelipwa fedha nyingi zaidi katika ya England kufuatia kujiunga na Sky Sports kama Balozi kuanzia mwakani.
  Dau lake atakalokuwa analipwa Sky inadaiwa ni zaidi ya lile analolipwa, Gary Neville, ambaye inaaminika anapata Pauni Milioni 1.2 kwa mwaka.
  Vipengele vya Mkataba wa Henry bado vinamruhusu kufanya kazi BBC katika mashindano makubwa kama alivyofanya nchini Brazil katika Kombe la Dunia. Lakini haruhusiwi kufanya kazi na wapinzani wa Sky, BT Sport, ambao walimtaka pia.
  Henry amestaafu soka mwezi uliopita nchini Marekani na wakati anacheza aliwika Arsenal na Barcelona akiwa mmoja wa wanasoka waliokuwa wanalipwa vizuri.
  Thierry Henry
  Thierry Henry
  Thierry Henry sasa ndiye mchambuzi anayelipwa fedha nyingi England baada ya kujiunga na Sky Sports
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: THIERRY HENRY APIGA BONGE LA BAO BAADA YA KUSTAAFU SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top