• HABARI MPYA

  Tuesday, December 16, 2014

  TAMBWE AWAPA AHADI NONO YANGA SC WAKITIMIZA SHARTI MOJA TU

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AMSHAMBULIAJI Mrundi, Amisi Tambwe ameomba mashabiki wa Yanga SC wampe sapoti ili aendeleze moto wake wa kufunga mabao katika soka ya Tanzania.
  Kauli ya Tambwe inakuja siku moja, baada ya kusaini Mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Yanga SC akitokea kwa mahasimu, Simba SC.
  “Ninafurahi kusaini Mkataba huu mzuri na timu yangu mpya, ninaomba mashabiki wa Yanga SC waniunge mkono, wanipe sapoti ili niendelee kufanya vizuri katika soka ya Tanzania, “alisema Tambwe akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya kusaini Simba SC. 
  Tambwe amesema anaifahamu Yanga SC siku nyingi na klabu ya kwanza kuchezea Tanzania ingekuwa hiyo, kwa sababu alifahamiana na kiongozi mmoja wa klabu hiyo, Francis Kifukwe muda mrefu.
  “Nilifahamiana na Kifukwe miaka minne au mitano iliyopita na alitaka nije kucheza Yanga SC, lakini haikufanikiwa hadi Simba SC wakanichukua,”amesema.
  Amisi Tambwe kushoto akiwa na Francis Kifukwe baada ya kusaini Yanga SC jana

  Ameongeza; “Mimi sasa hivi ni mchezaji wa Yanga SC, naelekeza fikra na mawazo yangu kwa mwajiri wangu mpya, nataka niwape raha mashabiki wa timu yangu mpya,”amesema.       
  Katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili wa dirisha dogo Tanzania, Tambwe alisaini jana Mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Yanga SC baada ya kuachwa Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAMBWE AWAPA AHADI NONO YANGA SC WAKITIMIZA SHARTI MOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top