• HABARI MPYA

  Wednesday, December 10, 2014

  SIMBA SC YASHUSHA WAKALI WAWILI WA THE CRANES, NI JUUKO NA SIMON SSERUNKUMA, WOTE TAYARI WAPO KAMBINI ZANZIBAR

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wawili wa waliokuwamo kwenye kikosi cha Uganda, The Cranes kilichocheza mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, beki Juuko Murushid na mshambuliaji Simon Sserunkuma wamejiunga na Simba SC kwa majaribio.
  Juuko aliwasili jana usiku Dar es Salaam, wakati Ivan ametua mchana wa leo pamoja na Nahodha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Joseph Owino.
  Kutua kwa wachezaji hao, kunapunguza nafasi ya Mkenya, David Owino ‘Calabar’ kusajiliwa kwenye kikosi cha Simba SC.
  Huyo ni kwa sababu Sserunkuma wa Express ya Uganda na Juuko aliyewahi kucheza soka ya kulipwa nchi za Asia, kwa sasa ni wachezaji huru, wakati kwa Owino Simba SC italazimika kuilipa klabu yake, Gor Majia.
  Juuko Murushid tayari yuko kambini Zanzibar

  BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba Owino amekwishatumiwa tiketi na Simba SC aje Tanzania, lakini amekuwa akikwamishwa na tatizo la usafiri.
  Aidha, pamoja na Simba SC kukubaliana na Mtibwa Sugar kuuziana beki Hassan Ramadhani Kessy, lakini mchezaji huyo ametaka dau kubwa ambalo Wekundu hao wa Msimbazi ‘wanajifikiria’ kutoa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASHUSHA WAKALI WAWILI WA THE CRANES, NI JUUKO NA SIMON SSERUNKUMA, WOTE TAYARI WAPO KAMBINI ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top