• HABARI MPYA

  Tuesday, December 16, 2014

  MICHUANO YA COPA COCA-COLA YAENDELEA KUTIMUA VUMBI

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  MICHUANO ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 ngazi ya Taifa inaendelea leo jioni (Desemba 16 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani.
  Uwanja wa Nyumbu uliopo mkoani Pwani utazikutanisha timu za Mjini Magharibi na Dodoma katika mechi ya kundi B, wakati kundi C kutakuwa na mechi kati ya Arusha na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
  Wakati kesho (Desemba 17 mwaka huu) ikiwa ni mapumziko, michuano hiyo itaingia hatua ya robo fainali keshokutwa (Desemba 18 mwaka huu) kwenye viwanja hivyo hivyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MICHUANO YA COPA COCA-COLA YAENDELEA KUTIMUA VUMBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top