// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MICHO: KUTOFANYIKA CHALLENGE PIGO KWA SOKA YETU CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MICHO: KUTOFANYIKA CHALLENGE PIGO KWA SOKA YETU CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 12, 2014

    MICHO: KUTOFANYIKA CHALLENGE PIGO KWA SOKA YETU CECAFA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Uganda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ amesema kukwama kufanyika kwa michuano ya Kombe la Challenge ni pigo kubwa kwa soka ya Afrika Mashariki na Kati.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana kwa simu kutoka Kampala, Uganda- kocha huyo wa zamani wa Yanga SC amesema kwamba anasikia machungu sana kutofanyika kwa michuano hiyo.
    Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limekosa nchi ya kufanya mashindano ya Challenge mwaka huu, baada ya Ethiopia waliopewa uenyeji awali kujitoa kwa sababu zao binafsi. 
    “Kama kocha wa kigeni niliyefanya kazi kwa muda mrefu CECAFA, inayoongoza soka ya Afrika Mashariki na Kati na kuendesha mashindano yote ya Challenge na Kagame (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati), naweza kusema mimi ni kocha nayefundsha Afrika ambaye ni zao la hayo mashindano,”amesema Micho.
    Micho amesema hiyo ndiyo sababu anajisikia uchungu sana kwa kutofanyika kwa mashindano hayo mwaka huu, akiamini ni pigo kwa soka ya ukanda huu.
    Kocha Micho kushoto amesema kwamba kutofanyika kwa Challenge mwaka huu ni pigo kubwa kwa soka ya Afrika Mashariki na Kati

    “Kwa miaka yote hiyo viongozi wa CECAFA wamefanikiwa mwaka hadi mwaka kufanikisha mashindano hayo na kukuza ubora wake, kutofanyika kwake mwaka huu ni pigo kubwa,”ameongeza Micho, anayefundisha Uganda, The Cranes. 
    “Sina haja ya kuhoji kwa nini Ethiopia wamejitoa na kwa nini hajapatikana mbadala wake, lakini nawaombea sana CECAFA wavuke salama katika kipindi hiki kigumu cha mpito na wafanikishe kufanya mashindano ya Challenge japokuwa muda umepita,”.
    Micho amesema mashindano hayo ni muhimu mno kwa nchi za ukanda wa CECAFA kujiandaa na michuano mingine mikubwa ya kimataifa kama CHAN 2016 itakayofanyika Rwanda, mechi za kufuzu Olimpiki 2016 mjini Rio de Janeiro na kufuzu Mataifa ya Afrika mwaka 2017. 
    “Naichukulia michuano ya Challenge kama uti wa mgongo wa soka ya Afrika Mashariki na Kati na kwa kiasi kikubwa mustakabali wa soka yetu umelalia kwenye mashindano hayo. Natumaini, juhudi na maarifa vitafanyika kunusuru mashindano haya,”amesema Micho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO: KUTOFANYIKA CHALLENGE PIGO KWA SOKA YETU CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top