• HABARI MPYA

  Wednesday, December 17, 2014

  BARCELONA YAADHIBU 8-1 KOMBE LA MFALME

  KLABU ya Barcelona imeshinda mabao 8-1 usiku wa jana dhidi ya Huesca katika mchezo wa kuwania kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Mfalme Uwanja wa Camp Nou.
  Kwa matokeo hayo, Barca imetinga 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 12-1, ambako itakutana na Elche au Valladolid mwezi Januari.
  Mabao ya Barca jana yalifungwa na Pedro matatu dakika ya 21, 26 na 44, Roberto dakika ya 29, Iniesta dakika ya 40, Adriano dakika ya 68, Traore daika ya 78 na Sandro dakika ya 84, wakati bao pekee la wapinzani lilifungwa na Galvez dakika ya 86.
  Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Masip, Montoya, Adriano/Douglas dk46, Bartra, Rafinha, Samper, Mascherano, Iniesta, Roberto, El Haddadi/Traore dk74 na Pedro/Sandro dk46.
  HUESCA: Jiminez, Moreno, Scardina/Morillas dk84, Galvez, Perez, Manolin, Sosa/Gaspar dk61, Bernal, Cabezas, Esnaider/Murillo dk71.
  Barcelona forward Adama Traore celebrates his goal which put the hosts 7-0 ahead
  Mshambuliaji wa Barcelona Adama Traore akishangilia baada ya kufunga bao la saba

  PICHA ZAIDI NENDAhttp://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2876481/Barcelona-8-1-Huesca-agg-12-1-Pedro-nets-hat-trick-Catalan-giants-cruise-through.html#ixzz3M8KkPVxK 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YAADHIBU 8-1 KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top