• HABARI MPYA

  Thursday, December 18, 2014

  AZAM FC YACHAPWA TENA UGANDA, YAPIGWA 1-0 NA URA

  MABINGWA wa Tanzania Bara, Azam FC jana wamepoteza mechi ya pili mfululizo katika ziara yao ya Uganda.
  Azam FC jana imechapwa bao 1-0 na URA mjini Kampala, baada ya awali kufungwa mabao 3-2 mwishoni mwa wiki na SC Villa.
  Azam FC iliyo chini ya makocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda, George ‘Best’ Nsimbe imeweka kambi Uganda kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyosimama kwa mwezi mmoja, ambayo itarejea wiki ijayo.
  Katika kambi hiyo ya siku 10, pamoja na mazoezi, Azam FC inacheza mechi za kirafiki ili kupima kikosi chake, baada ya usajili wa dirisha dogo.

  Katika dirisha dogo, Azam FC imewasajili beki Serge Wawa Pascal raia wa Ivory Coast aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan, Mganda Brian Majwega kutoka KCCA ya Kampala na Amri Kiemba kwa mkopo kutoka Simba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA TENA UGANDA, YAPIGWA 1-0 NA URA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top