• HABARI MPYA

  Friday, December 05, 2014

  AIRTEL YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO UDSM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vifaa vya michezo kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali yanayotegemea kuanza jumatatu ijayo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Mchango huu ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuendeleza michezo nchini inayodhirishwa kupitia mpango wake wa kuinua soka la vijana chini ya miaka 17 wa Airtel Rising Stars mpango ambao umewawezesha vijana wakitanzani na Afrika kwa ujumla kuonyesha uwezo wao wa kisoka na kuweza kufikia malengo yao.
  Akiongoe wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Leo tunatoa vifaa vya michezo ikiwemo seti 12 za jezi, shinguard, soksi, glovu za goalikipa pamoja na makombe yatakayowezesha kuendesha mashindano haya yanayoshirikisha wanafunzi kutoka vituvo mbalimbali chuoni hapa. Niwazi kwamba michezo ni burdani na ni sehemu ya kujenga mwili na afya hivyo ni muhimu pia kwa wanafunzi kutenga muda wao wa masomo na kushirikia katika michezo mbalimbali.  Natoa wito kwa wanafunzi wengi kujitokeza na kushiriki mashindano haya.”.

  Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akimkabidhi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/- mjini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.

  “Udhamini wetu leo ni mwanzo wa mkakati wa kutoa ofa kabambe itakayowapatia wanavyuo uhuru wa kuongea na kupata dhamani yamatumizi ya pesa zao.
  Ofa hii ya huduma maalumu ijulikanayo kama UN255 Itazinduliwa rasmi wakati wa kilele cha michuano hiii mwishoni mwa wiki ambapo wanafunzi watafurahi huduma zetu nyingi ikiwa ni pamoja na internet, ujumbe mfupi , kupiga simu kwa gharama nafuu. Aliongeza Mmbando
  Kwa upande wake Naibu Makamu mkuu wa chuo Profesa Yunus Mgaya alisema” nawashukuru sana Airtel kwa mchango wa mkubwa na kwa kutuwezesha kupata vifaa vya michezo zitavyotuwezesha kuvitumia muda wote wa mashindano. Sisi kama chuo hatukuwa na bajeti ya kununua vifaa hivi hivyo msaada huu umekuja kwa wakati muafaka hivyo nawapongeza sana Airtel kwa mchango wao.”
   “Vifaa hivi vitaleta tija kwa wanafunzi na kuinuua michezo chuoni hapa na ofa hii  UN255 itawawezesha wanafunzi na pamoja na  familia yetu yote ya chuo kikuu cha Dar es saalam kufurahia huduma za mawasiliano bora na kwa bei nafuu” aliongeza Mgaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AIRTEL YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO UDSM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top