• HABARI MPYA

    Friday, August 01, 2014

    FACUNDO FERREYRA ATUA NEWSCASTLE

    KLABU ya Newcastle United imekamilisha uhamisho wa mkopo wa Facundo Ferreyra kutoka Shakhtar huku ikiwa fursa ya kumsajili moja kwa moja kwa dau la Puni Milioni 6.5.
    Mshambuliaji huyo wa Argentina ataiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ya Alan Pardew Uwanja wa St James Park, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kukataa kurejea klabu yake halisi.
    Ferreyra alikuwa miongoni mwa wachezaji sita wa Shakhtar pamoja na Wabrazil Douglas Costa, Fred, Dentinho, Alex Teixiera na Ismaily ambao walishindwa kuripoti Ukraine kufuatia mchezo wa kirafiki dhidi ya Lyon nchini Ufaransa Jumamosi kutokana na vurugu za kisiasa Ukraine.

    Kifaa kipya: Facundo Ferreyra (kulia) amejiunga na Newcastle kwa mkopo kutoka Shakhtar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FACUNDO FERREYRA ATUA NEWSCASTLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top