• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 20, 2014

  ROONEY AKUBALI KUSAINI MKATABA MPYA MAN UNITED, LAKINI...

  MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amekubali mapendekezo ya Mkataba mpya utakaomuwezesha kuvuna Pauni 300,000 kwa wiki Manchester United, lakini hatasaini dili hilo vipengele vya kuhusu matumizi ya picha yake viweke sawa.
  Inafahamika mpachika mabao huyo United na wawakilishi wake wamefurahia Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na posho.
  Mshahara mnono: Wayne Rooney anaweza kusaini Mkataba mpya wa Pauni 300,000 kwa wiki United muda si mrefuBack: Rooney returned to training on Wednesday after the team's five-day break in Dubai
  Rooney alirejea mazoezini jana baada ya siku tano za timu kuwa mapumzikoni Dubai
  Pamoja na hayo, Rooney hawezi kusaini Mkataba huo hadi mambo kadhaa kuhusu haki za matumizi ya picha zake zieleweke.
  Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward anajiamini suala hilo linaweza kuwa limetatuliwa kabla ya kumalizika ya siku ya leo au kesho .
  Kama haitakuwa hivyo, itabidi isubiriwe hadi United itakaporejea kutoka Ugiriki kwenye mchi yao ya Ligi ya Mabingwa wiki ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROONEY AKUBALI KUSAINI MKATABA MPYA MAN UNITED, LAKINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top