• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 20, 2014

  AL AHLY WAIFUMUA SFAXIEN 3-2 MBELE YA MKWASA NA KUBEBA SUPER CUP

  Na Princess Asia, Cairo
  AL Ahly ya Misri imemuonyesha kocha wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa kwamba wao ni tishio, baada ya kuifunga mabao 3-2 CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa kuunganisha mataji Afrika, maarufu Super Cup uliofanyika Uwanja wa kimataifa wa Cairo usiku huu.
  Nimewasoma; Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa alikuwepo uwanjani leo kuishuhudia Al Ahly ikibeba Super Cup

  Mkwasa, Kocha Msaidizi wa Yanga alikuwepo uwanjani leo kuwashuhudia mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Ahly na mabingwa wa Kombe la Shirikisho, Sfaxien wakimenyana.
  Yanga SC itamenyana na Ahly katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa kwanza ukifanyika Dar es Salaam Machi 1 na marudiano wiki moja baadaye Cairo- na Mkwasa alikuwepo uwanjani leo ili kuwatathmini wapinzani wao hao.
  Si haba, Mkwasa ameona Ahly inafungikaje kupitia mabao mawili waliyopata Sfaxien na ameona mbinu zao za kutafutia mabao kupitia mabao yao matatu- hivyo anarejea Dar es Salaam na somo zuri kwa wachezaji wake kabla ya kumenyana na mabingwa hao wa kihistoria barani.
  Mabao ya Ahly leo yamefungwa na Gedo dakika ya 23 pasi ya Ahmed Fathy, Amr Gamal mawili dakika ya 54 pasi ya Abdalla El Said na dakika ya 69 pasi ya Yedan, wakati ya Sfaxien yamefungwa na Maaloul dakika ya 63 na Ben Youssef dakika ya 78 pasi ya 
  Kouyate.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY WAIFUMUA SFAXIEN 3-2 MBELE YA MKWASA NA KUBEBA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top