• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 19, 2014

  YANGA WAJIBU MAPIGO KWA AL AHLY, SHUSHUSHU LAO CHARLES BONIFACE MKWASA ‘MASTER’ TAYARI LIPO CAIRO

  Na Prince Akbar, Dar es Salaam
  YANGA SC wamejibu mapigo. Al Ahly walituma wawakilishi wao wiki mbili zilizopita Dar es Salaam kuja kuangalia timu hiyo ikimenyana na Komorozine ya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Na jana kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amepanda ndege kuelekea Cairo, Misri kushuhudia Al Ahly wakicheza mechi ya Super Cup dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, utakaofanyika kesho Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
  Mkwasa katika picha tofauti jana wakati anaondoka nyumbani kwake. Picha kwa hisani ya mke wa kocha huyo,Betty Mkwasa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dodoma.

  Al Ahly walikuja kutazama uchezaji na mbinu za Yanga ambao nao wamemsafirisha Mkwasa Cairo kwa ajili hiyo hiyo.
  Mkwasa anatarajiwa kurejea nchini Ijumaa kuungana na kikosi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi. 
  Yanga SC itamenyana na Al Ahly  Machi 1, mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA WAJIBU MAPIGO KWA AL AHLY, SHUSHUSHU LAO CHARLES BONIFACE MKWASA ‘MASTER’ TAYARI LIPO CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top