• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 24, 2014

  REAL YAZIACHA HATUA MOJA BARCA NA ATLETICO MBIO ZA UBINGWA LA LIGA

  TIMU ya Atletico Madrid jana ilikula ngwala katika mbio zake za ubingwa wa La Liga baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Osasuna, hivyo kuwaacha Real Madrid wajinafasi kileleni kwa pointi tatu zaidi.
  Mabingwa Barcelona na vinara Real walilazimishwa sare kwenye Uwanja wa Osasuna, El Sadar mjini Pamplona mapema msimu huu na Atletico ikadondoka jana.
  Alvaro Cejudo alifunga bao la kwanza dakika ya sita wakati makosa ya beki wa pembeni, Juanfran yalimruhusu Emiliano Armenteros kufunga bao la pili dakika ya 21 kabla ya Roberto Torres kufunga la tatu dakika ya 42. Atletico inabaki na pointi 60 sawa na Barcelona iliyo katika nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao, wakati Real pointi 63 juu yao.
  Majanga: Diego Costa na David Villa wakijiandaa kuanza mpira baada ya kufungwa moja ya mabao matatu ya jana na Osasuna
  All over: Roberto Torres nets the third for Osasuna before half-time
  Tumemaliza kazi: Roberto Torres akishangilia baada ya kufunga bao la tatu jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL YAZIACHA HATUA MOJA BARCA NA ATLETICO MBIO ZA UBINGWA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top