• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 20, 2014

  TENGA AMTEUA BILIONEA MULINDWA KUWA MAKAMU MPYA WA RAIS CECAFA

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  RAIS wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amemteua bilionea Lawrence Mulindwa wa Uganda kuwa Makamu mpya wa Rais wa bodi hiyo.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo na CECAFA, uteuzi huo umeanza jana Februari 19, 2014 na kilichomvutia Tenga, beki na Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni rekodi nzuri ya Mulindwa.
  Mabosi CECAFA; Leodegar Tenga kulia akiwa na Lawrence Mulindwa

  Mulindwa amekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) kwa mafanikio hadi Agosti mwaka jana alipojiuzulu na nafasi yake ikachukuliwa na Moses Hassim Magogo aliyeshinda uchaguzi.  

  Ni mdau mkubwa wa soka Uganda anayemiliki shule ambazo zinazalisha vipaji vya wanamichezo wengi Afrika Mashariki na Kati.
  Mapema mwaka huu ameinunua shule ya Kisubi High School kwa Sh. Bilioni 3 za Uganda wakati tayari anamiliki shule maarufu ya St Mary’s SS Kitende iliyoibua vipaji vya wanamichezo wengi wakiwemo Emmanuel Okwi, Joseph Owino, Tony Odur na wengineo.
  Baadhi ya wanamichezo wa Tanzania wa kimataifa pia wametokea katika shule hiyo mfano mchezaji wa timu za taifa za mpira wa kikapu na Netiboli, Sofia Komba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TENGA AMTEUA BILIONEA MULINDWA KUWA MAKAMU MPYA WA RAIS CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top