• HABARI MPYA

  Friday, February 28, 2014

  UCHAGUZI MKUU TASWA KUFANYIKA WATER FRONT

  Na Dina Ismail, Dar es Salaam
  UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika katika ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam keshokutwa, imeelezwa.
  Katibu Mkuu anayemaliza muda wake TASWA na ambaye atatetea nafasi hiyo Jumapili, Amir Mhando ameaiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, hiyo inafuatia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kujitolea kudhamini Mkutano huo.
  Mbali na NSSF, kampuni ya CXC ya Dar es Salaam na waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitolea pia kupiga tafu Mkutano huo Mkuu wa TASWA.
  Mwenyekiti anayemaliza muda wake TASWA, Juma Pinto ambaye atatetea nafasi yake Jumapili

  Mhando amsema NSSF imetoa udhamini wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja ametoa Sh Milioni 1 kwa ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
  “Tunashukuru Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam,  waandaaji wa Tamasha la Pasaka kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF wametusaidia kwa kiasi fulani mkutano wetu.
  “Bajeti yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama wa Dar es Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine wanatoka Morogoro, Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na kuongeza kuwa wanatarajia wanachama 150 washiriki mkutano huo.
  Alisema mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba wanachama kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari kwa mkutano huo wa aina yake.
  Watu 27 wanatarajiwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TASWA.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TASWA, Boniface Wambura aliwataja waliochukua na kurudisha fomu hizo hadi zoezi hilo lilipofungwa jana saa 9:00 Alasiri kuwa ni .
  Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.
  Mhazini Msaidizi ni Elius John Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija Richard Shija na Mohamed Salim Mkangara.
  Katibu Msaidizi ni Alfred Lucas Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Ptarick Raymond Nyembera. Katibu Mkuu ni Amir Ally Mhando pekee.
  Waombaji nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed Omary Masenga. Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John Ishabairu, Juma Abbas Pinto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UCHAGUZI MKUU TASWA KUFANYIKA WATER FRONT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top