• HABARI MPYA

  Wednesday, February 19, 2014

  RIVALDO MWENYE MIAKA 41 ACHEZA MECHI PAMOJA NA MWANAWE MWENYE MIAKA 18

  MSHINDI wa Kombe la Dunia na gwiji wa Brazil, Rivaldo ameweka historia baada ya kuonyesha picha akiwa na mwanawe uwanjani anayetumia jina la baba yaje huyo.
  Rivaldo, mwenye umri wa miaka 41, aliingia uwanjani akitokea benchi wakati Mogi Mirim wakitoa sare ya 1-1 na XV de Piracicaba katike mechi ya ligi ya jimbo la Sao Paolo Uwanja wa Romildo Ferreira.
  Ilikuwa mara ya kwanza anacheza sambamba na mwanawe huyo mwenye umri wa miaka 18, Rivaldo Junior.
  Kijana safi kabisa: Rivaldo amecheza uwanja mmoja na mwanawe, Rivaldo Junior wakati Mogi Mirim ikitoka sare na XV de Piracicaba

  Kinda Rivaldinho ana safari ndefu kama kweli anataka kufuata nyayo za baba yake, aliyejipatia umaarufu mkubwa kwenye soka.
  Katika mataji, Rivaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia maarufu kama Ballon D'Or mwaka 1999 katikati ya miaka yake mitano ya kuichezea Barcelona ambayo alishinda mataji ya UEFA Super Cup, mawili ya La Liga na Kombe la Mfalme.
  Aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002 kabla ya kwenda kuongeza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na vigogo wa Italia, AC Milan.
  Sealed with a kiss: Rivalo celebrates winning the World Cup with fellow Brazil hero Ronaldo
  Busu tamu: Rivaldo akisherehekea Kombe la Dunia na shujaa mwenzake wa Brazil enzi hizo, Ronaldo.

  Rivaldo, ambaye pia amechezea Santa Cruz, Corinthians, Palmeiras, Deportivo La Coruna, Cruzeiro, Olympiacos, AEK Athens, Bunyodkor, Sao Paulo, Kabuscorp na Sao Caetano, alirejea kwa mara ya pili Mogi Mirim Desemba mwaka jana ambako aliibukia kisoka. Pia ni rais wa klabu hiyo kwa sasa.
  Pick that out: Rivaldo scores a free-kick as Olympiacos lose a European tie at Liverpool in 2004
  Rivaldo akifunga kwa mpira wa adhabu wakati Olympiacos ikifungwa na Liverpool katika mechi ya michuano ya Ulaya mwaka 2004
  A bit special: Rivaldo scored an overhead kick for Barcelona in a 3-3 draw with Manchester United in 1998
  Rivaldo akifunga kwa tik tak Barcelona ikitoa sare ya 3-3 na Manchester United mwaka 1998
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RIVALDO MWENYE MIAKA 41 ACHEZA MECHI PAMOJA NA MWANAWE MWENYE MIAKA 18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top