• HABARI MPYA

  Thursday, February 27, 2014

  CHELSEA 1-1 NA GALATASARAY ULAYA

  CHELSEA imepata sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Galatasaray katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Bora Ulaya usiku huu.
  Fernando Torres alitangulia kuifungia The Blues dakika ya tisa na kuifanya Chesea kuwa timu ya kwanza ya England kufunga bao katika 16 ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, baada ya wiki iliyopita Arsenal kufungwa 2-0 na Bayern Munich na Manchester City kufungwa 2-0 na Barcelona, wakati jana Manchester United iIifungwa 2-0 pia ugenini na Olympiacos. 
  Hata hivyo, wenyeji Galatasaray walisawazisha bao hilo dakika ya 64 kupitia kwa Chedjou.
  Hatufungwi sisi; Fernando Torres akishangilia na wenzake baada ya kuifungia bao Chelsea usiku huu
  In a twist: Fernando Torres slots home with his foot at an extraordinary angle to give Chelsea an early lead
  Kitaalamu: Fernando Torres akiifungia bao la kuongoza Chelsea
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA 1-1 NA GALATASARAY ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top