• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 20, 2014

  WENGER AMPA MAKAVU ROBBEN, AMUAMBIA "BWANA UPARA UMETUBAKA MCHANA KWEUPE"

  KOCHA Arsene Wenger amemtuhumu Arjen Robben kujirusha na kumponza kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny kutolewa nje kwa kadi nyekundu, ambayo ilisababisha wafungwe mabao 2-0 na Bayern Munich.
  Mwalimu huyo Mkuu wa Arsenal pamoja na kulalamikia kitendo hicho, pia alisema wachezaji wengine wa Bayern walimtumia vibaya refa Nicola Rizzoli.
  "Kipa alimgusa kweli, lakini nilimuambia Robben aliongeza chumvi na ilibadilisha mchezo.
  "Siyo tu ilibadilisha mchezo, iliua mchezo. Ulikuwa mchezo wa ubora wa hali ya juu na katika kipindi cha pili ulikuwa unaelekea mwisho," alisema Wenger.
  Umejirusha? Arsene Wenger anafikiri hivyo - na amemuambia Arjen Robben hivyo wakati mchezo umesimama
  Eyes on the ball: Robben collects a high ball in the Gunners box as Szczesny stands his ground
  Macho kwenye mpira: Robben akipokea mpira wa juu katika eneo la hatari la The Gunners huku Szczesny akipiga hesabu za kuokoa
  Fou'? It looked like Szczesny clatters into Robben's standing leg taking him down
  Faulo? Inaonekana kama Szczesny anamkwatua mguuni Robben
  Crunch time: The duo collide, with referee Nicola Rizzoli awarding a penalty and sending the Pole off
  Wawili hao walienda chini wote na refa Nicola Rizzoli akatoa penalti na kadi nyekundu
  Airborne: Robben sails through the London skies after his collision with a stunned Szczesny
  Robben akiugulia maumivu huku Szczesny akimuangalia
  There may be trouble ahead: Robben cries out upon hitting the plush Emirates turf
  Robben alianguka chini wakati akigombea mpira ma kipa huyo wa kimataifa wa Poland, ambaye alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja. 
  Wenger alimnyooshea mikono Robben kumshutumu kwamba alijiangusha kutafuta penalti. David Alaba akakosa penalti hiyo, lakini wachezaji 10 wa Arsenal hawekuweza kuwazuia Toni Kroos na Thomas Muller kuifungia Bayern katika ushindi wa 2-0.
  Mesut Ozil pia alikosa penalti upande wa The Gunners na kuna hatari Szczesny akaadhibiwa zaidi na UEFA kwa kuonyesha ishara mbaya jukwaani baada ya kutolewa.
  Early bath: The Italian official moved swiftly to send Szczesny off
  Refa wa Italia akimuonyesha kadi nyekundu Szczesny iliyoimaliza Arsenal
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WENGER AMPA MAKAVU ROBBEN, AMUAMBIA "BWANA UPARA UMETUBAKA MCHANA KWEUPE" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top