• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 24, 2014

  YANGA SC NA SHOOTING YAINGIZA FEDHA NYINGI KULIKO SIMBA NA JKT RUVU

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  MECHI za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zilizohusisha timu za Yanga na Simba, na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zimeingiza jumla ya sh. 101,165,000.
  Yanga ambayo iibugiza Ruvu Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza sh. 68,450,000 kutokana na washabiki 11,972 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
  Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgao wa sh. 15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 10,441,525.42. Gharama za tiketi ni sh. 3,813,600 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata sh. 4,877,538.71. Uwanja sh. 8,129,231.19.
  Mrisho Ngassa kushoto na Emmanuel Okwi kulia waling'ara Yanga ikishinda 7-0 Jumamosi

  Gharama za mchezo zilikuwa sh. 4,877,538.71 wakati Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,438,769.36. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata sh. 945,110.
  Nayo mechi ya Simba na JKT Ruvu ilishuhudia na watazamaji 5,850 na kuingiza sh. 32,715,00 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 4,990,423.73.
  Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 7,428,742 wakati tiketi ni sh. 2,542,400 huku gharama za mechi zikiwa 2,266,395.86. Uwanja ulipata sh. 3,777,326.44 wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ni sh. 2,266,395.86.
  Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulipata mgawo wa sh. 1,133,167.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 881,376.17.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC NA SHOOTING YAINGIZA FEDHA NYINGI KULIKO SIMBA NA JKT RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top