• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2014

  AMIR KHAN ATEREMKA ULINGONI PAMBANO NA MAYWEATHER...KISA MIDHARAU YA MPINZANI WAKE

  BONDIA Amir Khan amekata tamaa ya kuzipiga na bingwa wa uzito wa Light-Middle, Floyd Mayweather Jnr kutokana na kile kinachoonekana kumkera, dharau za mpinzani wake.
  Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 27 alithibitisha Januari amesaini Mkataba kupigana na mkali huyo wa kutupa makonde mjini Las Vegas, lakini Mayweather ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwataka wafuasi wake waamue apigane na nani - bondia huyo wa Bolton au Marcos Maidana. 
  Pamoja na hayo, Khan amejibu katika tweets mfululizo jana usiku kwamba hatapigana na Mmarekani huyo ambaye hajawahi kupoteza pambano na sasa Mayweather ataelekeza nguvu zake kwa Maidana. 
  Amejitoa: Amir Khan amethibitisha hatapigana na Floyd Mayweather mjini Las Vegas
  It's a no: Khan has said the prospects of fighting Floyd Mayweather Jnr in May are non-existent
  Khan amesema uwezekano wa pambano na Floyd Mayweather Jnr Mei mwaka huu haupo
  Doesn't matter: Mayweather asked his fans who they wanted to fight him next as he defends a world title
  Haijalishi: Mayweather amewauliza mashabiki wake ni bondia gani wanataka apigane naye katika pambano lijalo la kutetea taji lake la dunia
  It's off: Khan confirms his fight with Mayweather will not be happening
  Imefutwa: Khan amethibitisha pambano lake na Mayweather halitakuwepo. "Hakuna majibu kutoka kwa Mayweather au timu yake. Pambano halitakuwepo. Ningechukua pambano la kuwania taji Desemba mwaka jana dhidi ya Alexander...,' Khan alitweet.
  Akaendelea tena kuandika: "Dharau kubwa sana na timu yake. Wamenipotezea muda. Bahati nzuri kwake Maidana, dhidi ya Mayweather.
  "Naweza kuomba radhi kwa maelfu ambao wamesikitishwa. Wewe, mimi na kila mmoja tulitaka pambano na Mayweather. Analeta upuuzi," alisema.
  Khan alitumai kwamba dili alilosaini Desemba lilimuweka kwenye nafasi ya kuzipiga na Mayweather. 
  Lakini wakati Mayweather amewaandikia wafuasi wake kwenye Twitter, majibu ya awali yanaonyesha kwamba Khan hatapanda ulingoni Mei 3.
  Asilimia themanini ya kura za mashabiki zimemchagua Maidana, ambaye ameshinda mapambano yake 35 kati ya 38.
  Inafahamika, Khan alimpiga Maidana kwa pointi mwaka 2010 walipokutana Las Vegas. 
  Impact felt: Khan, left, punches Marcos Maidana his victory in their WBA super lightweight fight in December, 2010
  Anastahili: Khan, kushoto, akimtupia konde Marcos Maidana katika pambano ambalo alishinda la uzito wa Super Light wa WBA Desemba mwaka 2010
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AMIR KHAN ATEREMKA ULINGONI PAMBANO NA MAYWEATHER...KISA MIDHARAU YA MPINZANI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top