• HABARI MPYA

  Saturday, February 22, 2014

  HATIMAYE ROONEY AJITIA PINGU MVUA TANO MAN UNITED, SASA NDIYE MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIA NZIMA

  MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amemshukuru kocha David Moyes jana usiku baada ya kujihakikishia mustakabali wake katika klabu ya Manchester United, kufuatia kusaini Mkataba mpya wa miaka mitano ambao utamfanya apate mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki.
  Rooney aliwaambia United alitaka kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kutofautiana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England walilazimika kupambana na ofa ya dau la Pauni Milioni 30 kutoka Chelsea.

  Rasmi: Rooney amethibitisha kusaini kwake Mkataba mpya United kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema 'furaha sana'Sorted: Rooney (centre) with executive vice chairman Ed Woodward and manager David Moyes
  Wa hapa hapa: Rooney (katikati) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Ed Woodward na kocha David Moyes jana baada ya kusaini Mkataba mpya
  Moyes alisema jana namna ambavyo alimshawishi mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kubaki Old Trafforf alipokutana naye katika kikao chake cha siri kilichofanyika Juni mwaka jana.

  MALIPO MAPYA YA ROONEY

  Pauni 15,600,000 kwa mwaka
  Pauni 300,000 kwa wiki
  Pauni 43,000 kwa siku
  Pauni 1,800 kwa saa
  Pauni 30 kwa dakika
  50p kwa sekunde
  Na Rooney ametoa shukrani zake kwa kocha wake huyo aliyemuibua Everton baada ya kusaini Mkataba ambao utamalizika Juni mwaka 2019 ambao unamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani.
  Alisema: "Kulikuwa kuna tetesi kibao wakati wa majira ya joto, lakini nilitulia wakati David Moyes alipokuja kwenye klabu.
  "Nimekuwa na uhusiano mzuri naye na anaonyesha imani kubwa kwangu. Mazungumzo yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu – Nina furaha kusaini sasa.
  "Hii ni moja ya klabu kubwa duniani na fahamu kwamba nitacheza hapa kwa sehemu kubwa ya maisha yangu ya soka, ni kitu ambacho nasonga mbele kwa ajili hiyo. Nina furaha kwamba kila kitu sasa kimemalizwa na ninaweza kuelekeza fikra zangu kwenye soka yangu,"alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATIMAYE ROONEY AJITIA PINGU MVUA TANO MAN UNITED, SASA NDIYE MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIA NZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top