• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 24, 2014

  HII YA MAYWEATHER NDIO KUFURU HASWA, ACHANA NA FEDHA NDUGU

  BONDIA Floyd Mayweather amewaonyesha mamilioni ya wafuasi wake kwenye Twitter namna alivyosherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake mwishoni mwa wiki kwa kupanda ndege binafsi na rafiki zake na timu ya walinzi wake kwenda kufanya 'kufuru'.
  Mayweather, ambaye ameripotiwa kuachana na demu wake Shantel Jackson, alikuwa amezungukwa na marafiki kibao wa kike wakati akiangalia mechi ya mpira wa kikapu, Los Angeles Lakers ikiifunga Boston Celtics jana jioni.
  Bingwa huyo mara nane wa dunia ambaye hajawahi kupoteza pambano anatarajiwa kupanda ulingoni Mei 3, lakini si kama ilivyotarajiwa awali angepigana na Muingereza, Amir Khan mjini Las Vegas baada ya kuwaambia wafuasi wake kwenye Twitter wapige kuraa apigane na nani kati ya Khan au Muargentina Marcos Maidana.

  Self-promotion: Team Mayweather take to the sky as the fighter celebrates his 37th birthday in customary fashion
  Jeuri ya fedha: Timu la Mayweather likiwa angani kwenda kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa bondia huyo
  Having fun: Mayweather was pictured with three women - he is rumoured to have split from Shantel Jackson
  Vimwana wakali: Mayweather akiwa amezungukwa na vimwana licha ya taarufa ameachana na mpenzi wake Shantel Jackson
  Bet it tastes rich; This cake - celebrating his favourite things - was made for Mayweather's birthday last year

  Mambo ya fedha; Keki hii maalum ilitengenezwa kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa Mayweather mwaka jan
  The green man: Mayweather poses for a picture with his favourite thing - a large pile of cash
  Mtu Pesa: Mayweather akiwa amepozi kwa picha na burungutu la fedha
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HII YA MAYWEATHER NDIO KUFURU HASWA, ACHANA NA FEDHA NDUGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top