• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2014

  JOHN TERRY AIBEBA CHELSEA ENGLAND

  BAO la dakika ya mwisho kabisa la Nahodha aliyerejea John Terry limeipa Chelsea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton jioni hii katika Ligi Kuu ya England.
  Ilikuwa kama Jose Mourinho tayari amekwishapoteza pointi mbili katika mbio za ubingwa kutokana na timu hizo kuwa hazijafungana hadi Phil Jagielka alipomchezea rafu Ramires.
  Frank Lampard akaenda kupiga mpira wa adhabu  ambao uliguswa na Branislav Ivanovic na Terry akateleza kwenda kuusukumia nyavuni dhidi ya kipa Tim Howard.
  Baada ya ushindi huo wa mbinde unaoifanya Chelsea itimize pointi 60 baada ya mechi 27 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, na The Blues watasafiri hadi Galatasaray kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Hatua ya 16 Bora Jumatano.

  Mkombozi: Frank Lampard (kushoto) na John Terry ushirikiano wao umeipa bao la ushindi ChelseaQuick off the mark: John Terry reacts first as Slyvain Distin, Leighton Baines and Phil Jagielka can only watch
  John Terry alikuwa wa kwanza kuugusa mpira huku Slyvain Distin, Leighton Baines na Phil Jagielka wakiangaliaThe late show: John Terry slides in front of Tim Howard as Chelsea seal a dramatic late win
  John Terry akiteleza kufunga dhidi ya Tim Howard 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JOHN TERRY AIBEBA CHELSEA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top