• HABARI MPYA

  Wednesday, February 19, 2014

  SHAABAN RAMADHANI KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR, BAUSI NJE

  Na Salum Vuai, Zanzibar
  CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimemtangaza Shaaban Ramadhan kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Zanzibar Heroes.
  Jukumu la kwanza la kocha huyo, litakuwa kuteua wachezaji na kuwaandaa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia la linaloshirikisha nchi ambazo si wanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ‘VIVA World Cup’.
  Kalenda ya bodi inayosimamia michuano hiyo, inaonesha kuwa patashika hizo mwaka huu zitafanyika nchini Sweden mwezi wa Mei.
  Kocha Shaaban Ramadhani kushoto akiwa Rais wa ZFA, Ravia Idarous kulia na rais wa zamani wa ZFA, Ali Ferej Tamim

  Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina, amethibitisha uteuzi huo ambao alisema umepata baraka za kamati tendaji ya chama hicho iliyokutana hivi karibuni kujadili mambo mbalimbali.
  Aidha, chama hicho kimemteua Hafidh Muhidin kuwa msaidizi wa kocha huyo.
  Kocha Shaaban Ramadhan, ambaye wakati akicheza mpira alikuwa mshambuljai tishio katika timu ya Navy na baadae ilipobadilishwa jina na kuitwa KMKM, alikuwa msaidizi wa Hafidh Badru wakati Zanzibar ilipoandika historia kwa kutwaa ubingwa wa Chalenji kwa mara ya kwanza mwaka 1995 nchini Uganda. 
  Uteuzi huo unamaanisha Salum Bausi aliyeiongoza Zanzibar Heroes mara mbili katika mashindano ya Chalenji (mwaka 2011/12 na 2013/14) nchini Uganda na Kenya mtawalia, ameenguliwa kwenye nafasi hiyo.
  Zanzibar ilishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya dunia ya VIVA mwaka 2009, wakati ngarambe hizo zilipofanyika nchini Kurdistan Irak Kaskazini, na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHAABAN RAMADHANI KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR, BAUSI NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top