• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 19, 2014

  PRISONS YAIRARUA JKT RUVU 6-0 SOKOINE, KUSHUKA SASA LABDA!

  Na Jackline Charles, Mbeya
  PRISONS FC imeendelea vyema na kampeni zake za kuepuka kushuka daraja baada ya kuifumua JKT Ruvu mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jioni hii. 
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Omega Seme, Nurdin Chona, Lugano Mwangama, Peter Michael mawili na Frank ‘Lampard’ na sasa Wajelajela wanashusha pumzi ndefu baada ya ushindi huo unaowaweka katika nafasi nzuri kidogo kwenye msimamo wa ligi. 
  Kikosi cha Prisons kimefanya mauaji leo Mbeya

  Matokeo hayo yanaifanya Prisons ipande hadi nafasi ya 10 kutoka ya 14, baada ya kutimiza pointi 16 ikizishusha Ashanti United yenye pointi 14 nafasi ya 11, JKT Oljoro pointi 14 pia nafasi ya 12, JKT Mgambo pointi 14 pia nafasi ya 13 na Rhino Rangers pointi 13 nafasi ya mwisho walipokuwa wao.  
  Prisons imerudi vizuri mzunguko wa pili ikiwa chini ya kocha mpya mkongwe nchini David Mwamwaja na huu ni mchezo wa tatu mfululizo wanashinda hivyo kufufua matumaini ya kubaki Ligi Kuu.
  Aliyekuwa kocha wa Prisons katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Jumanne Challe amehamia Rhino Rangers ambayo sasa inaburuza mkia katika Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRISONS YAIRARUA JKT RUVU 6-0 SOKOINE, KUSHUKA SASA LABDA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top