• HABARI MPYA

  Wednesday, February 26, 2014

  ADAKE NANI YANGA JUMAMOSI, KASEJA AU DIDA?

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  JUMA Kaseja alidaka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa Yanga SC ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Komorozine ya Comoro Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hiyo ikiwa mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa.
  Aanze huyu? Juma Kaseja hakufungwa Yanga ikishinda 7-0 dhidi ya Komorozine
  Deogratius Munishi ‘Dida’ akapangwa katika mchezo wa marudiano mjini Moroni na kufungwa mabao mawili, Yanga ikishinda 5-2.
  Au aanze huyu? Deogratius Munishi 'Dida' alidaka vizuri Yanga ikishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting
  Jumamosi, Yanga itacheza na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Hatua ya 16 Bora Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na katika kikosi cha kwanza, sehemu pekee ambayo inawaumiza vichwa wengi ni langoni.
  Aanze Dida au Kaseja? Yanga SC ilimsajili makusudi Kaseja kutokana na uzoefu wake wa mechi kubwa za kimataifa, ikiamini atawasaidia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
  Lakini tayari kuna mitazamo tofauti juu ya mlinda mlango huyo wa zamani Simba SC, wengine wakiamini uwezo wake umeshuka na wengine wakiamini bado yuko sawa na anaweza kufanya kazi nzuri.
  Dida alidaka vizuri Yanga SC ikishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi iliyopita, lakini huo ulikuwa mchezo wa Ligi ya Bara, alifungwaje mabao mawili Comoro?

  Pamoja na yote, benchi la Ufundi la Yanga SC chini ya kocha wake Mkuu, Hans van der Pluijm litaibuka na jibu sahihi Jumamosi, nani ataanza. We unafikiri nani, Kaseja au Dida?
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ADAKE NANI YANGA JUMAMOSI, KASEJA AU DIDA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top