• HABARI MPYA

  Friday, February 21, 2014

  POGBA AITAKATISHA JUVE ULAYA, SPURS YAKALISHWA...SWANSEA DROO

  MSHAMBULIAJI wa Southampton, Dani Osvaldo aliifungia bao la kwanza Juventus anayoichezea kwa mkopo katika ushindi wa mabao 2-0 kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Trabzonspor mjini Turin jana.
  Katika mchezo huo wa kwanza hatua ya 32 Bora, Mtaliano huyo alifunga bao lake hilo la kwanza dakika ya 15 tangu ajiunge na klabu hiyo Januari baada ya kumtoka beki Jose Fonte.
  Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba aliihakikisha ushindi Juve kwa bao la dakika ya mwisho kabisa.
  Ushindi: Dani Osvaldo (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Juventus katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Trabzonspor
  Watch this Moyes! Former Manchester United midfielder Paul Pogba (L) scored a second in injury time
  Angalia hii Moyes! Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba (kushoto) alifunga bao la pili dakika za majeruhi

  Katika mchezo mwingine, Jonathan Soriano alifunga katika ushindi wa Salzburg dhidi ya Ajax mabao 3-0 mjini Amsterdam.
  Soriano alifunga mara mbili la kwanza dakika ya 14 kwa penalti na la pili dakika ya 35 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Ajax, Jasper Cillessen na lingine likafungwa na Sadio Mane.
  Lazio pia ilipata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ludogorets ya Bulgaria.
  Johnny be good: Jonathan Soriano celebrates after scoring a brace for Salzburg against Ajax
  Jonathan Soriano akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Ajax

  Roman Bezjak alifunga bao la ushindi katika mchezo ambao timu zote zilikosa penalti na zote kupoteza wachezaji kwa kadi nyekundu.
  Wageni walikosa penalti dakika ya nane kupitia kwa Svetoslav Dyakov, na Felipe Anderson akapoteza nafasi ya kuisawazishia Lazio dakika tano tangu kuanza kipindi cha pili.
  Dyakov alitolewa kwa kadi nyekundu dakika tano baadaye, lakini idadi ikaongezeka baada ya Luis Cavanda kutolewa pia nje dakika ya 73.
  Eintracht Frankfurt ilitoka nyuma kwa mabao mawili na kupata sare ya 2-2 na Porto.
  Mabao ya kila kipindi ya Ricardo Quaresma na Silvestre Varela yaliiweka mbele timu ya Ureno, lakini Joselu akapunguza moja dakika ya 72 kabla ya Alex Sandro kujifunga dakika sita baadaye na kuwapa Wajerumani hao sare ya ugenini.
  Mchezaji wa Valencia aliyetokea benchi alibadilisha mchezo kwa mabao mawili ya dakika za lala salama yaliyoleta ushindi wa 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev.
  Portugeezer: Ricardo Quaresma helped give Porto a 2-0 lead before drawing with Eintracht Frankfurt
  Ricardo Quaresma alifunga katika sare ya 2-2 ya Porto na Eintracht Frankfurt

  Eduardo Vargas na Sofiane Feghouli, wote wakiingia kipindi cha pili walifunga katika dakika za 80 na 90 na kuiweka barabarani timu hiyo ya Hispania katika mbio za taji hilo la Ulaya.
  Mechi hiyo ilichezwa mjini Nicosia, Cyprus, kwa sababu ya vurugu zinazoendelea katika Jiji hilo la Ukraine .
  Fiorentina pia iliifumua mabao 3-1 Esbjerg, Alessandro Matri akiifungia timu hiyo ya Serie A bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Martin Pusic kusawazisha dakika mbili baadaye, Josip akafunga la pili dakika ya 15 kwa Wataliano hao.
  Italian job: Ex-Liverpool misfit Alberto Aquilani (C) scored to give Fiorentina a commanding 3-1 win over Esbjerg
  Mchezaji wa zamani wa Liverpool, misfit Alberto Aquilani (katikati) alifunga katika ushindi wa Fiorentina wa 3-1 dhidi ya Esbjerg

  Alberto Aquilani akafunga la tatu kwa penalti kabla ya mapumziko na kuivusha mguu mmoja mbele hatua ya 16 Bora La Viola.
  Sevilla ilitoa sare ya 2-2 na Maribor ikitoka nyuma kwa mabao 2-1.
  Marcos Tavares aliwafungia Waslovenia bao la kuongoza, lakini jitihada za kipindi cha pili za Kevin Gameiro na Federico Fazio zikabadilisha matokeo.
  Dare Vrsic aliyetokea benchi akawasawazishia wenyeji dakika ya 81.
  On the spot: Spurs captain Michael Dawson (R) reacts after seeing the penalty go in past Brad Friedel
  Penalti: Nahodha wa Spurs, Michael Dawson (kulia) akisikitika baada ya mkwaju wake wa penalti kutoka nje ya lango la Brad Friedel

  Bao la dakika ya 81 la Yevhen Konoplyanka kwa penalti liliipa Dnipro ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham nchini Ukraine.
  Timu nyingine ya Ukraine, Shakhtar Donetsk pia itakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Viktoria Plzen.
  Stanislav Tecl aliifungia bao la kuongoza timu ya Czechs dakika ya 62, lakini Luiz Adriano akasawazisha dakika nne baadaye.
  Rubin Kazan waliomaliza 10 walipata sare ya 1-1 ugenini na Real Betis, licha ya Alexander Prudnikov kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 28.
  Wakati huo tayari Betis wanaongoza kwa bao la Didac Vila, lakini Roman Eremenko akasawazisha kwa penalti dakika ya 74.
  Benfica ilishinda 1-0 dhidi ya PAOK Salonika, shukrani kwake mfungaji wa bao hilo Rodrigo Lima kipindi cha pili, wakati AZ Alkmaar ilipata ushindi kama huo mbele ya Slovan Liberec, bao pekee la Nick Viergever dakika ya 89.
  Mechi baina ya Chornomorets na Lyon na Anzhi Makhachkala na Genk ziliisha kwa sare ya bila kufungana, huku Anzhi ya Urusi ikimaliza mchezo na wachezaji 10 kufuatia Ilya Maksimov kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 89.
  Mechi baina ya Swansea na Napoli na Maccabi Tel-Aviv na Basle pia ziliisha kwa sare ya 0-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA AITAKATISHA JUVE ULAYA, SPURS YAKALISHWA...SWANSEA DROO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top