• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2014

  ROONEY, VAN PERSIE WAING'ARISHA MAN UNITED ENGLAND

  SIKU moja baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka mitano utakaomfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani, Pauni 300,000 kwa wiki, Wayne Rooney amewafurahisha Manchester United kwa kufunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace ugenini katika Ligi Kuu ya England usiku huu.
  Wauwaji; Van Persie kushoto na Rooney anayefuatia wameifungia United leo katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace

  Mholanzi Robin van Persie alifunga bao la kwanza dakika ya 62 kwa penalti, kufuatia Chamakh kumchezea rafu Patrice Evra kwenye eneo la hatari. 
  Dakika sita baadaye, Muingereza Rooney akawainua vitini mashabiki wa United kwa bao safi la pili baada ya kupokea pasi ya Evra.
  Ushindi huo, unaifanya United itimize pointi 45 baada ya kucheza mechi 27 na inarejea nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROONEY, VAN PERSIE WAING'ARISHA MAN UNITED ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top