• HABARI MPYA

    Friday, February 28, 2014

    MECHI YA SIMBA NA PRISONS YASOGEZWA MBELE

    BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na moja ya Ligi Daraja la Kwanza (VPL).
    Mechi namba 143 kati ya Tanzania Prisons na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu sasa imesogezwa kwa siku moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile Machi 8 mwaka huu Mbeya City itautumia uwanja huo kwa mechi nyingine ya VPL.
    Simba SC

    Nayo Mgambo Shooting iliyokuwa icheze na Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga sasa imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka huu kwa vile Kituo cha Tanga kitakuwa na mechi mbili.
    Kwa upande wa FDL, mechi ya Mkamba Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa Machi 3 mwaka huu badala ya Machi 9 mwaka huu mjini Ifakara. Mechi hiyo imerudishwa nyuma ili kuipunguzia gharama Kimondo SC kwani Machi 1 mwaka huu itacheza na Burkina Faso mjini Morogoro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA SIMBA NA PRISONS YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top