• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 22, 2014

  FURAHA YAREJEA ARSENAL, MTU APIGWA NNE KAMA KASIMAMA

  MSHAMBULIAJI Olivier Giroud amerejea na kuisaidia Arsenal kushinda mabao 4-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya Englandf usiku huu.
  Mshambuliaji huyo wa Ufaransa ambaye aliachwa benchi katika mechi mbili zilizopita kutokana na kushuka kiwango na kashfa ya ngono- alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza wakati The Gunners wakijisahaulisha kipigo cha Bayern Munich katikati ya wiki katika Ligi ya Mabingwa. Mchezaji ghali wa klabu hiyo, Mesut Ozil alipumzishwa leo.
  Kiungo wa Czech, Tomas Rosicky alifunga bao la tatu, kabla ya Laurent Koscielny kuhitimisha karamu ya mabao ya timu hiyo.
  Sunderland, ambaye itakutana na Manchester City katika Fainali ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup Uwanja wa Wembley wikiendi ijayo, ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Emanuele Giaccherini aliyetokea benchi. 
  Ushindi huo, unakifanya kikosi cha Arsene Wenger kitimize pointi 59 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
  Furaha imerudi: Laurent Koscielny (katikati) akisherehekea baada ya kufunga kwa pamoja na Oliver Giroud (kushoto) na Per Mertesacke
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FURAHA YAREJEA ARSENAL, MTU APIGWA NNE KAMA KASIMAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top