• HABARI MPYA

    Monday, February 17, 2014

    FABREGAS ATANGULIZA SALAMU MANCHESTER BARCELONA WAKIWA KWENYE NDEGE KUIFUATA CITY KWA MPAMBANO WA KESHO LIGI YA MABINGWA

    WAPO njiani. Cesc Fabregas ameweka kwenye picha kwenye akaunti yake ya Instagram wakiwa kwenye ndege leo Jumatatu na wachezaji wenzake wa Barcelona kuelekea England kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi Manchester City.
    Ameposti picha akiwa na wachezaji wenzake Alex Song, Carles Puyol na Gerard Pique wakati ndege inataka kuruka mabingwa hao wa Hispania wakienda jiji la Manchester kwa ajili ya mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora, itakayopigwa Uwanja wa Etihad.
    Wakiwa wamevalia suti za kimichezo nyekundu, wachezaji hao walionekana vizuri na walio tayari kwa mpambano huo mgumu wa ugenini.
    Tayari kuondoka: Cesc Fabregas ameposti picha hii katika Instagram yake akiwa na Alex Song, Gerard Pique na Carles Puyol kwenye ndege kwa ajili ya mechi dhidi ya City kesho usiku

    Barcelona inakwenda kwenye mechi hiyo ikitoka kuichapa mabao 6-0 Rayo Vallecano Jumamosi katika La Liga, matokeo ambayo yanawafanya waendelee kukabana koo na Real Madrid na Atletico kileleni.
    Lakini watakutana na Manchester City ambayo pia iko vizuri, ikiwa imetoka kuing'oa Chelsea katika Raundi ya Tano ya Kombe la FA mwishoni mwa wiki na kocha Manuel Pellegrini, ambaye ana uzoefu wa kucheza na Barca, anajiamini City inaweza kufanya vizuri katika mchezo huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FABREGAS ATANGULIZA SALAMU MANCHESTER BARCELONA WAKIWA KWENYE NDEGE KUIFUATA CITY KWA MPAMBANO WA KESHO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top