• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 25, 2014

  AZAM KUJIULIZA KWA ASHANTI UNITED KESHO DAR

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
  Mechi itazikutanisha timu za Azam inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 37 dhidi ya Ashanti United iliyoko nafasi ya 12 kwa pointi zake 14.
  Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewaagiza wanachama wake- vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwapatia orodha ya klabu zote za mpira wa miguu zilizosajiliwa katika mikoa yao.
  Kikosi cha Azam FC

  Orodha hiyo inatakiwa kujumuisha namba ya usajili wa klabu, viongozi waliopo madarakani kwa sasa pamoja na mawasiliano yao (namba za simu na anuani za email) na eneo yalipo makao ya klabu husika.
  Kwa utaratibu huo, vyama vya mikoa vitakusanya taarifa za klabu zinazocheza ligi ya mikoa, lakini wakati huo vinatakiwa kuwasiliana na wanachama wake (vyama vya wilaya) kupata taarifa za klabu zinazocheza ligi za wilaya na baadaye kuziwasilisha TFF.
  Klabu ambazo taarifa zake zitakuwa hazijawasilishwa TFF hadi Agosti mwaka huu hazitaruhusiwa kushiriki ligi ya msimu wa 2014/2015 katika ngazi yoyote ile.
  Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya programu ya mpira wa miguu kwa vijana.
  Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM KUJIULIZA KWA ASHANTI UNITED KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top