• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 17, 2014

  JANUZAJ AITWA TIMU YA TAIFA YA KOSOVO

  KINDA Adnan Januzaj amepigiwa simu na Naibu Waziri Mkuu wa Kosovo kuombwa aichezee mechi ya kwanza ya kimataifa nchi hiyo.
  Behgjet Pacolli, bilionea mmiliki kampuni za ujenzi anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 550, anajaribu kumshawishi Januzaj acheze dhidi ya Haiti mwezi ujao.
  Januzaj, mwenye umri wa miaka 19, badohajaamua acheze nchi gani soka ya kimataifa, lakini familia yake ilikuwa moja ya wanaharakati wa uhuru wa nchi hiyo.
  Wito Kosovo: Kosovo imemkaribisha mchezaji wa Manchester United, Adnan Januzaj aichezee timu yao ya taifa

  Pamoja na hayo, Kosovo bado haijapata uanachama wa FIFA, wameruhusiwa kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Haiti mwezi ujao.
  Januzaj alizaliwa mjini Brussels, Ubelgiji lakini kuna utata mkubwa juu ya mustakabali wake katika soka ya kimataifa.
  England ni moja ya nchi ambazo zinatumaini kumpata Januzaj.
  Breakthrough: Januzaj burst on to the Premier League stage with both goals in a 2-1 win at Sunderland earlier in the season
  Tishio jipya: Januzaj alianza kutisha katika Ligi Kuu ya England mapema msimu huu kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 wa United dhidi ya Sunderland
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JANUZAJ AITWA TIMU YA TAIFA YA KOSOVO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top