• HABARI MPYA

  Wednesday, February 19, 2014

  MASHALI, KASEBA WASAINI MKATABA WA KUZIPIGA MACHI 29 DAR

  Na Prince Akbar, Dar es Salaam
  MABONDIA Thomas Mashali na Japhet Kaseba wamesaini makubaliano ya kucheza  pambano la ubingwa wa Mabaara wa Universal Boxing Organization (UBO), pambano litakalopigwa Machi 29, mwaka huu katika ukumbi wa Karume, zamani ukiitwa PTA. 
  Pambano hilo linaandaliwa na Mratibu mashuhuri katika masuala ya ngumi za kulipwa nchini, hususani pande za Tanga, Ally Mwanzoa aliyefurahishwa na nidhamu iliyoonyeshwa na mabondia hao wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa makubaliano katika ukumbi wa Vijana, kinondoni, Dar es Salaam leo.
  Marasta kuzipiga; Japhet Kaseba kulia anaishi Kinondoni na Mashali anaishi Manzese, katikati ni promora wa pambano hilo, Ally Mwanzoa akiwatambulisha leo

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, kiongozi wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Kamwe aliyefuatana na Anthony Ruta amesema makubaliano yamekwenda vizuri na wote wametia saini kupigana katika uzito wa Middle.
  Mabondia wote wamechukua malipo yao ya awali kuashiria kuwa pambano hilo lipo na kila mmoja amejigamba kumchakaza mwenzake siku hiyo na kujitengenezea mazingira mazuri katika ubingwa wake huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHALI, KASEBA WASAINI MKATABA WA KUZIPIGA MACHI 29 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top