• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 26, 2014

  AZAM YAREJEA KILELENI LIGI KUU, MWAIKIMBA ARUDI NA MOTO

  Na Princess Asia, Dar es Salaam
  AZAM FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ashanti United jioni hii Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ifikishe pointi 40 baada ya kucheza mechi 18, ikiishusha nafasi ya pili, Yanga SC yenye pointi 38 ingawa ina mechi moja mkononi.
  Gaudence Exavery Mwaikimba alifunga kila kipindi dhidi ya timu yake ya zamani, mabao yote akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mganda, Brian Umony.
  Mwaikimba kushoto
  Beki Aggrey Ambroce Morris alifunga kwa penalti bao la kwanza la Azam baada ya kipa wa Ashanti United, Juma Mpongo kumchezea rafu Umony na Mwaikimba akafunga la pili akimalizia krosi ya Mganda huyo pia.
  Beki Said Morad ‘Mweda’ aliiadhibu pia timu yake ya zamani kipindi cha pili akiunganisha kona iliyochongwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ kabla ya Mwaikimba kuhitimisha karamu ya mabao ya Azam kwa bao safi la nne akiuwahi mpira uliotemwa na kipa Mpongo baada ya shuti la Umony.
  Ikumbukwe Mwaikimba alipangwa leo kwa sababu washambuliaji chaguo la kwanza la kocha Joseph Marius Omog, John Bocco ni majeruhi na Kipre Tchetche alikuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM YAREJEA KILELENI LIGI KUU, MWAIKIMBA ARUDI NA MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top