• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 24, 2014

  KENYA WENYEJI CHAN 2018, CAN MOROCCO MWAKANI

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeiteua Kenya kuandaa Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee mwaka 2018.
  Kwa mujibu wa taarifa ya CAF iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo, hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CAF chini ya rais wake, Issa Hayatou, kilichofanyika Ijumaa ya Februari 21 makao makuu ya bodi hiyo, Cairo, Misri. 

  “Kamati Kuu ya CAF imeipa Kenya haki za kuandaa Fainali za mwaka 2018 za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), kufuatia kuhakikishiwa na serikali ya nchi hiyo kwamba watafanya kwa ufanisi,” imesema taarifa ya CAF.
  Kikao hicho pia kimesema Fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (CAN) zitafanyika Morocco mwakani na fainali zitachezwa kuanzia Januari 17 hadi Februari 7, katika miji ya Rabat, Agadir, Tangier na Marrakech. 
  Jumla ya nchi 51 zinatarajiwa kushiriki, nchi 21 za juu kwenye viwango vya ubora zitaanzia kwenye hatua ya makundi, wakati nyingine zitaanzia kwenye mchujo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KENYA WENYEJI CHAN 2018, CAN MOROCCO MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top