• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 21, 2014

  TABATA KUMUENZI STRAIKA CHANGA KWA BONANZA LA MAANA JUMAPILI SHULE

  Na Dina Ismail, Dar es Salaam
  TIMU ya Tabata Veterans, imeandaa bonanza maalum la kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Omary Changa aliyefariki dunia mwezi uliopita, ambalo litafanyika Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Tabata Shule, Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tabata Veterans, Rodgers Peter ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba maandalizi yote ya bonanza hilo la kutathmini mchango wa mwenzao huyo aliyetangulia mbele ya haki yamekwishakamilika.
  Kimwili umetutoka, koroho bado tupo nawe; Omary Changa wa pili kulia waliosimama baada ya Kudra Omary katika kikosi cha Yanga cha mwaka 2004 makao makuu ya klabu hiyo Jangwani. Wanaomfuatia ni Noel Pompy, Salum Swedi na Omar Kapilima. Walioinama kutoka kulia ni Ramadhani Wasso, Freddy Mbuna, Ally Mayay, Abdul Mtiro, Athumani Majani na Said Maulid 'SMG'. 

  “Maandalizi yamekamilika na tunatarajia litakuwa bonanza zuri na sehemu nzuri ya watu kukutana na kukumbuka kuhusu Omary Changa, ambaye alikuwa mtu wa watu kwa kweli,”alisema Peter.
  Peter alisema bonanza hilo litakaloanza saa 2:30 asubuhi, litahusu michezo mbalimbali ikiwemo soka na litafuatiwa na burudani nyingine baadaye kabla ya kufungwa Saa 12:00 jioni.
  Peter amewaomba wadau na wapenzi wa soka Tabata kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuungana na wenzao kumuenzi marehemu Changa, ambaye enzi zake alichezea Yanga SC, Moro United na Kagera Sugar ya Bukoba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TABATA KUMUENZI STRAIKA CHANGA KWA BONANZA LA MAANA JUMAPILI SHULE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top