• HABARI MPYA

  Friday, February 28, 2014

  ETOILE SASA WATAKA KULIPWA BILIONI 3.1 ISHU YA OKWI, WAPO KIZIMBANI FIFA LEO

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  ETOILE Sportive du Sahel ya Tunisia imefufua kesi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mganda, Emmanuel Okwi, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), safari hii ikitaka kulipwa fidia ya Euro Milioni 1.5 sawa na Sh. Bilioni 3.1 za Tanzania.
  Kwa mujibu wa habari kutoka Zurich, Usiswi makao makuu ya FIFA, E.S.S. wanakwenda Zurich leo kujadili suala la mchezaji huyo wakiwa tayari wamesema wanataka walipwe Euro Milioni 1.5.
  Lakini E.S.S. inataka fedha hizo zilipwe na klabu ya SC Villa ya Uganda, ambayo ilimuuza mchezaji huyo Yanga SC.
  Bilioni 3? Etoile du Sahel inataka Euro Milioni 1.3 sawa na Sh. Bilioni 3.1 kutoka SC Villa ilyomuuza Emmanuel Okwi Yanga SC

  “Wanakwenda leo Zurich kujadili suala hili, wameitaka FIFA kuiagiza klabu ya Uganda, kulipa Euro Milioni 1.3 kutoka sehemu ya fedha walizopata kwa kumuuza mchezaji huyo Yanga SC,”kimesema chanzo kutoka FIFA.
  Ikumbukwe Okwi alisajiliwa Etoile akitokea Simba SC ya jijini Dar es Salaam tangu Januari 2013 kwa dau la Dola za Kimarekani 300,000 zaidi ya Sh. Milioni 480 za Tanzania.
  Hata hivyo, baada ya miezi mitatu mchezaji huyo aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya Tunisia, Etoile ikimtuhumu Okwi kuchelewa kurejea kazini baada ya ruhusa ya kwenda kuitumikia timu yaTaifa ya Uganda (Uganda Cranes).
  Okwi aliyapangua madai hayo kwa kusema klabu hiyo ilishindwa kumlipa mishahara kwa miezi mitatu mfululizo na akafanikiwa kuishawishi FIFA imruhusu kujiunga na SC Villa ili kulinda kiwango chake wakati suala lake likitafutiwa ufumbuzi.
  Hata hivyo, Desemba mwaka jana Villa ikamuuza Okwi Yanga SC ambapo ameidhinishwa kuendelea na kazi, huku Etoile ikiifufua kesi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ETOILE SASA WATAKA KULIPWA BILIONI 3.1 ISHU YA OKWI, WAPO KIZIMBANI FIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top