• HABARI MPYA

  Sunday, February 23, 2014

  CHOKY AIBUKA UKUMBINI NA GARI LA KUBEBEA WAGOINJWA, AFANYA BONGE LA SHOO DAR LIVE AKIPIGWA TAFU NA BANZA STONE, MUUMINI

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  UZINDUZI wa albamu ya Mtenda Akitendewa ya bendi ya Extra Bongo usiku wa jana umefana kwenye ukumbi wa Dar Live, maarufu kama Uwanja wa Taifa wa Burudani, Mbagala, Dar es Salaam.
  Kivutio zaidi kilikuwa kiongozi wa bendi ya Extra, ‘Kamarade’ Ally Choky aliyeingia ukumbini na gari la kukimbizia wagonjwa mahututi hospitali, maarufu kama Ambulance ukumbini.
  Ambulance hiyo ilisindikizwa na pikipiki zaidi ya 30 zile ambazo mjini tunaziita bodaboda, ambazo zilipofika mbele ya jukwaa zilifanya fujo za kutosha hadi mojawapo kudondoka na kumjerujhi dereva wake.
  Wapinzani wa zamani; Ally Choky kushoto akiimba na Banza Stone jana Dar LIve
  Ally Choky akishuka kwenye Ambulance
  Ambulance ya Choky ilivyopokelewa ukumbini
  Ajali; Boda boda hii ilikula mwereka na kujeruhi dereva wake

  Choky aliibuka kwenye mlango wa Ambulance akiwa peke yake na kupanda jukwaani moja kwa moja kuanza kuimba.
  Kwa kiasi fulani ilikumbushia enzi zile za msisimko wa muziki wa dansi  nchini kwa kiwango cha juu gwiji huyo alipokuwa akiingia ukumbini na Farasi, TingaTinga na kadhakika na kusababisha mpinzani wake mkuu enzi hizo, Banza Stone ampige kijembe “Kwenye Starehe Kijiko kimeingiaje”.
  Lakini jana Banza hakuwa mpinzani wa Choky, bali alikuwa mmoja wa wanamuziki waliyeimba naye jukwaa moja pamoja na Prince Mwinjuma Muumini ‘Kocha wa Dunia’ na bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) upande wa Taarab. 
  Choky alipagawisha mashabiki kwa nyimbo kadhaa zilizosindikizwa na sebene la nguvu lililokuwa linapikwa na wataalamu wa ala wakiongozwa na Ephraim Joshua katika gita la besi.
  Utamu zaidi katika shoo zilizovurumishwa na wanenguaji mahiri na wasiozeeka viuno wakiongozwa na Super Nyamwela na Maria Sharapova.
  Choky na mnenguaji wake
  Choky na Muumin Mwinjuma
  Maboda boda yakiongoza msafara wa Choky
  Wanenguaji wakifanya yao jukwaani
  Bin Zubeiry anapendwa na wengi sehemu nyingi,hapa nikiwa na mshakj wa Global Publisher kitengo Mawasiliano, ambaye ni kati ya wanaoendesha tovuti ya Global
  Viongozi wa makundi ya TMK Wanaume Halisi, King Kiboya kulia na TMK Wanaume Family Said Fela kushoto walikuwepo
  Mashujaa Bendi wakifanya yao jukwaani
  Khadija Kopa TOT kushoto akipagawisha mashabiki
  Amini na Linah kushoto wakifanya yao jukwaani

  Kabla ya Choky kupanda jukwaani, bendi ya TOT Taarab ikiongozwa na Malkia Khadija Omar Kopa na Abdul Misambano ‘Super Rocky’ ilikata utepe na baadaye wakapanda Mashujaa kabla ya wanamuziki wa Bongo Fleva Fleva Amin na Linah kutoka THT kuvamia jukwaa.
  Idadi ya watu waliohudhuria onyesho hilo haikuwa kubwa sana, lakini si haba kwa hadhi ya sasa ya Choky na wote waliomsindikiza viliendana na ukumbi ulipendeza kiasi chake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHOKY AIBUKA UKUMBINI NA GARI LA KUBEBEA WAGOINJWA, AFANYA BONGE LA SHOO DAR LIVE AKIPIGWA TAFU NA BANZA STONE, MUUMINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top