• HABARI MPYA

  Wednesday, February 19, 2014

  MARSH AFANYIWA UPASUAJI MKUBWA WA KOO LEO, DUA KWAKE TAFADHALI

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Sylvester Marsh leo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa koo katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.
  Upasuaji huo umegharimiwa na mmiliki wa hoteli ya Sapphire Court, iliyopo Kariakoo, Dar es Salaam ambaye aliamua kujitolea kufanya hivyo baada ya kufika hospitali kumjulia hali kocha huyo na kukuta hana msaada wowote.
  Hali ya Marsh ni mbaya na mwishoni mwa wiki alitembelewa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wadau wengine akiwemo Jamal Rwambo.
  Kila la heri koha; Sylvester Marsh leo anafanyiwa uoasuaji. Watanzania tumuombee dua auvuke mtihani salama. Amin.

  Lakini inasikitisha tu, TFF haijamsaidia lolote kocha huyo ambaye amefanya kazi za TFF kwa takriban miaka 10 sasa. 
  Marsh alianza kuwa Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania mwaka 2003 chini ya Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ kabla ya mwaka 2006 kupandishwa timu ya wakubwa, akianza kumsaidia Mbrazil, Marcio Maximo na baadaye Wadenmark, Jan Poulsen na Kim Poulsen.
  Kijana mdogo roho safi; Milionea Abdulfatah Salim Saleh amesaidia matibabu ya Marsh. Mungu amjaalie kwamoyo wake safi wa kujitolea.

  Marsh amekuwa akikataa hadi ofa za klabu mbalimbali ili aendelee kuitumikia timu ya taifa, lakini pamoja na yote TFF imeshindwa kuona thamani yake wakati huu mgumu kwake.
  Bin Zubeiry Blog inamtakia kila la heri Marsh katika siku hii ngumu zaidi maishani kwake leo. Auvuke salama mtihani huo wa upasuaji na apate ahueni,ili arejee kwenye shughuli za ujenzi wa taifa. Amin.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARSH AFANYIWA UPASUAJI MKUBWA WA KOO LEO, DUA KWAKE TAFADHALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top